• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Mara yapaa Kimichezo

20 July 2019

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Kighoma Malima, amesema kuwa pamoja na Mkoa wake kufanya vibaya katika matokeo ya mtihani wa kitaifa kidato cha sita mwaka huu lakini bado kuna fursa ya kufanya vizuri zaidi katika mitihani ijayo ya kitaifa.

Akipokea vikombe vya ushindi kwa michezo ambayo timu za Mkoa wa Mara zilipata kwenye mashindano ya Umisseta na Umitashumita mwaka huu, Malima amesema kuwa Mkoa  bado una nafasi ya kufanya vizuri endapo kila mmoja wetu atatimiza majukumu na wajibu wake kama inavyotakiwa. Ni lazima mikakati, ufuatiliaji na usimamizi wa nidhamu kwa walimu na wanafunzi vifanyike kwa ukaribu zaidi ili kuweza kupiga hatua kutoka hapa tulipo , alisema Malima.

Aidha ,Malima aliwataka walimu Mkoani Mara kujipanga vizuri ili kuhakikisha kuwa Mkoa unafanya vizuri kitaaluma kwa manufaa ya watoto wa Mkoa wa Mara na taifa kwa ujumla. “Haiwezekani tuwe tunafanya vizuri katika Michezo lakini kwenye taaluma tunashika mikia. Ni lazima Mkoa ujipange ili jitihada zilizotumika katika kuhakikisha Mkoa unafanya vizuri kwenye michezo ya Umisseta na Umitashumita iliyofanyika kitaifa Mkoani Mtwara na kupelekea Mkoa wa Mara kuwa mshindi wa tatu kitaifa zitumike pia katika kuhakikisha kuwa Mkoa unafanya vizuri kitaaluma na kupandisha ufaulu katika mitihani ya kitaifa kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari.”alisisitiza Malima.

Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Afisa elimu wa Mkoa wa Mara Bw. Emmanuel Kisongo amesema licha ya kufanya vizuri katika Michezo ,Mkoa umeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha ufaulu unapanda  kwenye mitihani ijayo ya kitaifa.

“Ni kweli kuwa hatujafanya vizuri kwenye taaluma kama Mkoa  na hilo halina ubishi ,lakini tunajipanga na kuendelea kusisitizana kila mmoja wetu awajibike anapostahili ili tutokane na aibu hii.”alisema Kisongo.

Mkoa wa Mara ni Mkoa mkongwe ambapo muasisi wa taifa hili Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere alizaliwa.Ni moja ya Mikoa iliyoka kanda ya ziwa.

Imeandaliwa na 

Stephano Amoni

Afisa Habari –Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.