Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 18/2/2025 amempokea na kuzungumza na Mkuu wa Utumishi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Marco Gaguti na ujumbe wake waliopo katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Mara.
Akizungumza katika mapokezi hayo yaliyofanyika ofisini kwake, Mhe. Mtambi amesema hali ya usalama ya Mkoa wa Mara ni shwari na wananchi wanaendelea kufanya shughuli zao za kawaida za maendeleo.
Mhe. Mtambi amelipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kazi nzuri wanayoifanya kulinda amani na usalama wa nchi na hususan katika maeneo ya mipaka ya Tanzania.
Mhe. Mtambi amelishukuru JWTZ kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Serikali ya Mkoa na kuahidi kuwa viongozi na Kamati ya Usalama ya Mkoa itaendelea kutoa ushirikiano kwa JWTZ katika utekelezaji wa majukumu yao katika Mkoa wa Mara.
Kwa upande wake, Meja Jenerali Gaguti akizungumza katika mapokezi hayo amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mara na Kamati ya Usalama ya Mkoa kwa kuhakikisha hali ya amani na utulivu inakuwepo katika Mkoa wa Mara jambo ambalo amesema linawawezesha wananchi kuendelea na shughuli zao za kujiletea kimaendeleo.
“Kutokana na amani na utulivu uliopo, wananchi wanaendelea kufanya shughuli zao za kujiletea maendeleo bila ya kuwa na hofu ya aina yoyote ile” amesema Meja Jenerali Gaguti.
Meja Jenerali Gaguti amemshukuru Mkuu wa Mkoa na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara kwa ushirikiano wanaoutoa katika jeshi hilo
Meja Jenerali Gaguti na ujumbe wake wapo katika ziara ya kawaida ya kikazi kwa siku mbili katika Mkoa wa Mara kuanzia leo na akiwa katika ziara hiyo ameambtana na maafisa mbalimbali kutoka makao makuu ya JWTZ.
Mapokezi hayo yamehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Gerald Musabila Kusaya, Mshauri wa Mgambo wa Mkoa wa Mara, Mkuu wa Kikosi cha JKT Rwamkoma, Mkuu wa Kambi ya JWTZ Makoko.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa