• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi akemea uvuvi haramu Mara

Posted on: February 17th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 17 Februari, 2025 amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Kwikuba, Kata ya Busambara, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na kuwakemea watu wote wanaojihusisha na uvuvi haramu katika Ziwa Victoria.

Mhe. Mtambi pia amewataka wananchi wote wa Mkoa wa Mara kuungana na kukemea uvuvi haramu na kutoa taarifa zinatazowezesha kuwakamata wanaojihusisha na uvuvi haramu katika ziwa Victoria ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Wanachokifanya ni kuhujumu misingi ya kiuchumi ya wananchi wote wanaotegemea Ziwa Victoria na mwisho wake tunajitengenezea umaskini na Serikali ya Mkoa wa Mara haitakubali hilo litokee” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amesema Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara inajjiandaa kufanya operesheni maalum ya kudhibiti uvuvi haramu katika Ziwa Victoria hivi karibuni na itawachukulia hatua za kisheria watu wote wanakaojihusisha na uvuvi haramu watakaokamatwa katika operesheni hiyo.

Mhe. Mtambi amesema kwa sasa kuna tishio la kumalizika kwa samaki katika Ziwa Victoria kutokana na uvuvi haramu na matokeo yake upatikanaji wa samaki umepungua na kupelekea baadhi ya viwanda vilivyokuwepo kufungwa na kuwahamasisha wananchi kuwabaini, kuwakemea na kutoa taarifa kwa viongozi kuhusiana na watu wanaojihusisha na uvuvi haramu.  

Mhe. Mtambi amewahakikishia wananchi kuwa uvuvi haramu usipokuwepo, samaki watarudi katika eneo hilo na itakuwa rahisi kuvishawishi uwekezaji wa viwanda vya samaki katika Mkoa wa Mara ambavyo vitanunua samaki pia kutoka eneo hilo.

Kanali Mtambi amesema kwa sasa Serikali inakamilisha upanuzi na ukarabati wa Uwanja wa Ndege Musoma ambao unaweza kurahisisha usafirishaji wa samaki kutoka Mkoa wa Mara kwenda maeneo mengine nchini na nchi jirani na wavuvi kuwawezesha wavuvi kupata soko la uhakika.

“Uwekezaji huu wa Serikali hauna maana kama matumizi ya ndege zitakazokuja Musoma itakuwa ni kwa ajili ya kusafirisha abiria tu bila ya kuwepo na uhakika wa mizigo yoyote kutoka Mkoa wa Mara” amesema Mhe. Mtambi.

Wakati huo huo, Mhe. Mtambi amewataka wananchi kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kufanya siasa za kiustarabu na kuwahakikishia kuwa Serikali ya Mkoa wa Mara imejipanga kulinda amani na usalama wakati wote wa uchaguzi.

Mhe. Mtambi amewataka wanasiasa wa Mkoa wa Mara kujenga hoja, kuelezea sera za vyama vyao na kuacha kuwalazimisha wananchi kumchagua mgombea wanayemtaka wao.  

Mhe. Mtambi ametumia pia fursa hiyo kumpongeza mbunge wa Musoma Vijijini Mhe. Prof.  Sospeter Muhongo kwa juhudi zake za kuwaletea wananchi wa eneo hilo maendeleo na hususan katika sekta za elimu, afya na kilimo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Juma Chikoka amesema Wilaya hiyo imeanzisha operesheni maalum ya kupambana na wavuvi haramu na wamejipanga kutokomeza tatizo hili ili kurejesha mazalia ya samaki katika aeneo hilo.

“Operesheni hii itawagusa wengi wanaojihusisha kwa namna moja au nyingine na uvuvi haramu” na kuongeza kuwa “tunawakaribisha wote wenye taarifa za watu wanaojihusisha na uvuvi haramu ili tuweze kuzifanyika kazi na kuwachukulia hatua za kisheria” amesema Mhe. Chikoka.

Mhe. Chikoka amesema Wilaya ya Musoma kwa sasa imeamua kutoa kipaumbele zaidi katika shughuli za uwekezaji ikiwemo kilimo, uvuvi, ufugaji na uchimbaji wa madini ambazo ni shughuli muhimu za wananchi wa hiyo.

Mhe. Chikoka amesema katika mikopo ya vikundi vya wananwake, vijana na watu wenye ulemavu miradi ya uzalishaji mali imepewa kipaumbele ili kuwezesha uzalishaji mali katika maeneo makubwa ya kiuchumi. 

Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mtambi afungua kambi ya madaktari bingwa na bobezi 64 Mara

    June 23, 2025
  • Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mara wapatiwa mafunzo

    June 20, 2025
  • Mara mshindi wa pili UMITASHUMTA 2025

    June 18, 2025
  • Zingatieni miongozo ya kilimo cha tumbaku- Dkt. Haule

    June 18, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa