Katika mwaka 2025, jumla ya watahiniwa 4,741 waliosajiriwa kufanya mtihani wa kidato cha sita katika Halmashauri tisa za Mkoa wa Mara wanaanza kufanya mtihani leo.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu Bwana Makwasa Bulenga imesema kuwa Mkoa una Shule za Sekondari 29 zenye wanafunzi wa Kidato cha Sita waliosajiriwa kufanya mtihani huo katika mikondo 144.
Aidha, Bwana Bulenga amesema Mkoa wa Mara pia una jumla ya watahiniwa 630 kutoka vyuo vitatu vya ualimu watafanya mtihani wao wa Taifa sambamba na mtihani wa Kidato cha Sita.
Vyuo vya ualimu vilivyopo katika Mkoa wa Mara ni Chuo cha Ualimu Tarime, Chuo cha Ualimu Bunda na Chuo cha Utalii Musoma ambavyo vina wanafunzi katika fani mbalimbali za mafunzo ya Ualimu.
Bwana Bulenga ameeleza kuwa maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwepo kutoa semina kwa wasimamizi wa mitihani na kusambaza vifaa vya mitihani katika Halmashauri, shule na vyuo vinavyohusika na mtihani huo.
Ratiba iliyotolewa na Baraza la Mtihani wa Taifa (NECTA) inaonyesha kuwa mtihani huo unafanyika kuanzia leo tarehe 05 Mei, 2025 hadi tarehe 26 Mei, 2025 hapa nchini.
Sekretarieti ya Mkoa wa Mara inawatakia wanafunzi wote wa Kidato cha Sita na Vyuo vya Ualimu mtihani mwema.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa