• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Waganga wa Wilaya Tembeleeni vituo vya kutolea Huduma- Dr. Besigwe

Posted on: January 18th, 2021

Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma Mkoa wa Mara Dr. Fabian Byesigwa amewataka Waganga Wakuu wa Wilaya pamoja na Waratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma Mkoa wa Mara kuacha tabia ya kukaa ofisini na kusubiri kuletewa taarifa badala yake wanapaswa  kwenda kutembelea vituo vinavyotoa huduma ili kuona hali ya  utendaji kazi katika vituo hivyo na  namna gani wanaweza kusaidia kutatua changamoto zinazokwamisha juhudi  za kutokomeza maambukizi ya  Kifua Kikuu na Ukoma Mkoani Mara.

Dr. Byesigwa ametoa kauli hiyo jana wakati wa  kikao cha kupitia na kurekebisha Takwimu za Kifua Kikuu na Ukoma Mkoa wa Mara kinachofanyika kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa Uwekezaji Mjini Musoma na kujumuisha Waganga Wakuu wa Wilaya, Makatibu wa Afya, Waratibu wa Kifua kikuu na Ukoma pamoja na wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.

Amesema kuwa, kuna haja ya Waganga Wakuu wa Wilaya kuacha tabia ya  kukaa ofisini na kusubiri kuangalia taaarifa kwenye mfumo na kusahau wajibu wao kuwa wao ndio wasimamizi wa masuala yote ya afya katika Halmashauri na Wilaya, hivyo wanapaswa  kutembelea maeneo yote hatarishi yanayodhaniwa ni kisababishi cha maambukizi ya kifua kikuu ambapo kwa kufanya hivyo kutasaidia kujua mwenendo wa maambukizi ya ugonjwa na kuweza kufanya  tathmini sahihi ya namna gani mikakati ya kudhibiti Kifua Kikuu inaendana na mazingira halisi.

Amesema kuwa, hali ya maambukizi ya kifua kikuu na Ukoma kwa sasa  kimkoa ni wastani lakini watumishi hawapaswi kuridhishwa na matokeo hayo badala yake waongeze bidii katika uwajibikaji kwa kuendelea kuibua wagonjwa na kuwapatia matibabu na pia kuhakikisha taarifa zote zinaingiza kwenye mfumo kwa usahihi ili ziweze kusaidia kuona wapi kuna changamoto na namna gani changamoto hizo zinaweza kutatuliwa kwa wakati.

Aidha ameongeza kusema kuwa madaktari wote wanapaswa kutumia weledi na taaluma zao vizuri katika kufanya uchunguzi kwa wagonjwa ili kuweza kupata majibu yenye tija yatakayosaidia kuibua na kutoa matibabu stahiki kwa wagonjwa ili kupunguza kasi ya ueneaji na vifo vitokanavyo na Kifua Kikuu na Ukoma.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Butiama Dr. Suke ameshauri kuwa ili kuhakikisha tunadhibiti Kifua Kikuu lazima viongozi wote katika ngazi ya chini kutafuta mikakati endelevu ya kuthibiti Kifua Kikuu badala ya kusubiri maelekezo kutoka ngazi za juu ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza yasitekelezeke kwa wakati kulingana na mazingira ya eneo husika.

Amesema,kifua kikuu  ni ugonjwa unaodumu kwa muda mrefu na kuua wagonjwa wengi japokuwa chanjo zipo na zinatolewa kwa wananchi, hivyo kama viongozi  tunapaswa tufanye ufuatiliaji wa kina kwa wagonjwa wanaoibuliwa na pia kufanyike tathmini ya huduma za uchunguzi zinazotolewa na madaktari kwa wagonjwa ili kujua chanzo hasa cha tatizo hili kuendelea kuwepo na namna gani tunalitatua.

Sambamba na hilo Dr. Byesigwa ametoa wito kwa jamii pamoja na maduka ya dawa  binafsi kushiriki katika harakati za kutokomeza Ugonjwa huu kwa sababu Kifua Kikuu ni ugonjwa unaotibika na pindi wanapoona mtu ana dalili za kifua kikuu basi ashauriwe kwenda katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa uchunguzi na matibabu sahihi badala ya kujificha ama kutumia dawa pasipo ushauri wa wataalamu wa afya.

Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kusaya awataka wahanga kutumia misaada kuboresha maisha

    May 19, 2025
  • BASATA yaijengea uwezo Mkoa wa Mara

    May 15, 2025
  • Mara kutumia fursa zilizopo kuboresha sanaa kwa vijana

    May 15, 2025
  • RC aipongeza Musoma ushindi wa ubora wa huduma za afya Kitaifa

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa