• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC Mara aunda Kamati kuchunguza ratiba za mabasi madogo

Posted on: October 27th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 26 Oktoba, 2025 amekutana na kuzungumza na maafisa na wadau wa usafirishaji wa Mkoa wa Mara katika ukumbi wa uwekezaji na kutoa siku 14 kuanzia leo kwa kamati aliyoiunda kukagua changamoto ya ratiba ya mabasi madogo yanayofanya shughuli zake katika Mkoa wa Mara.

Mhe. Mtambi ameunda kamati hiyo baada ya kupokea malalamiko ya Ndugu Yohana Lucas wa Kampuni ya Mabasi ya Nyawambu Express yanayofanya shughuli zake kutoka Stendi ya Musoma kwenda Busekela katika Wilaya ya Musoma kauli ambayo imeungwa mkono na wadau wengi wa usafirishaji walioshiriki kikao hicho.

“Ninataka niipate taarifa ya Kamati yenu ndani ya siku 14 ili Serikali ya Mkoa wa Mara iweze kuchukua hatua kuhusiana na changamoto hii” amesema Mhe. Mtambi na kuwataka wadau kuendelea na shughuli zao wakati Serikali inalifanyia kazi suala hilo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Mtambi amesema Kamati hiyo itaongozwa na Kamanda wa Kikosi cha Barabarani (RTO) Mkoa wa Mara Dezidery W. Waigwa, Wakili wa Serikali Mwandamizi Ndugu Kitia Turoke, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mhandisi Vedastus Maribe, Ndugu Ameir Mussa kutoka Kampuni ya Mabasi ya Nakajungu ambaye atakuwa mwakilishi wa wadau wa usafirishaji.   

Mhe. Mtambi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara amewataka madereva kuwa na leseni za udereva muda wote wakiwa kazini na amepiga marufuku tabia za askari kuwanyang’anya madereva leseni za udereva katika Mkoa wa Mara.

Mhe. Mtambi amewaagiza wamiliki wa vyombo vya usafirishaji kuhakikisha magari yao yapo kamili na vifaa vyote vinavyotakiwa kuwepo kwenye magari hayo vinafanyakazi kwa mujibu wa sheria kabla ya magari hayo hayajaingia barabarani. 

Mhe. Mtambi amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kutoa elimu kwa wadau wa usafirishaji na hususan madereva kuhusiana na sheria za usalama wa barabarani mara kwa mara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Kanali Mtambi amemuagiza Kamanda wa zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara kukagua stendi ya Bweri na kupeleka taarifa ya ukaguzi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma na nakala Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ili kufuatilia utekelezaji wa yatakayobainika katika ukaguzi huo.  

Mhe. Mtambi amewashukuru wadau wa usafirishaji kwa kutekeleza majukumu yao vizuri na namna ambavyo wanasaidia kuchangamsha uchumi na kuboresha huduma za usafirishaji katika Mkoa wa Mara.

Akitoa malalamiko yake mbele ya Mkuu wa Mkoa, Bwana Yohana Lucas amesema kampuni yake ina mabasi mawili, waliomba muda wamabasi yake kufanyakazi na akapewa na akalipia kibali cha muda huo, baada ya muda akaambiwa muda wa gari moja imepewa gari nyingine na kupewa muda mwingine.

Bwana Lucas amesema baada ya kuanza kuutumia muda huo, akaanza kufanyiwa fujo na kampuni nyingine wakidai kuwa ni muda wao na LATRA ikasema kampuni yake ndio ibadilishiwe muda wa usafiri na kampuni yake ikalazimika kutoa gari moja barabarani.

Bwana Lucas amesema kuwa kwa sasa gari moja iliyopo barabarani nayo muda iliyokuwa imepewa inaambiwa sio wake na hivyo magari yake yote yanatakiwa kutoka barabarani na yeye hana biashara nyingine amewekeza katika magari.  

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Usafirishaji Mkoa wa Mara Ndugu Suleiman Mataso, Makamu Mwenyekiti wa Usafirishaji Mkoa wa Mara amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kukubali kukutana na wadau wa usafirishaji Mkoa wa Mara ili kupokea changamoto zao.

Ndugu Mataso amezitaja changamoto zao kuwa ni pamoja na maaskari kuwaandikia faini nyingi kwa  kosa moja, ukaguzi wa mara kwa mara wa leseni, magari kufanya makossa nje ya Mkoa na kukamatwa ndani ya Mkoa wa Mara na maaskari kuwaandikia faini hewa.  

Aidha, wadau hao wamewalalamikia Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Mara kuwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya bodaboda na bajaji hayana usimamizi mzuri, sheria za upimaji wa samaki ni kandamizi kwa wenye vyombo vya usafiri, stendi ya Majita ni mbovu lakini wanalipa ushuru na wamelalamikia stendi ya Bweri kuwa haina mitaro, taa hakuna, ufinyu wa njia za magari kupita kuingia na kutoka stendi.

Bwana Mataso amesema kuwa wadau hao pia wamelalamikia LATRA kufanya upendeleo katika utoaji wa muda kwa mabasi, nauli ni ndogo ukilinganisha na umbali na hali ya barabara na hazijabadilika mpaka sasa kwa miaka 10 wamekuwa wakilalamikia.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Stanley Kajuna amesema Mkoa wa Mara una magari ya kubebea wagonjwa ya Serikali 31 ambayo yapo katika Halmashauri zote za Mkoa wa Mara.

Ndugu Kajuna amesema wagonjwa wa kawaida na wagonjwa wa Mama wajawazito na watoto wachanga wanahudumiwa na magari ya kubebea wagonjwa ya Serikali na madereva jamii wenye mikataba na Serikali na ili kupata huduma hiyo wagonjwa wanatakiwa kupiga namba ya simu ya bure 115.  

Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Agustine Boniphace Magere amesema mfanyabiashara anaponunua gari za abiria anatakiwa kwa mujibu wa sheria kulipeleka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kuweka vifaa vya zimamoto na uokoaji kuweka vifaa vya zimamoto na uokoaji.

Kamanda Magere amewataka wafanyabiashara wa magari kuzingatia matakwa hayo ya kisheria.

Katika usafirishaji kuna viashriria vya usafiri baadhi ya madereva wanabeba na mafuta ndani ya gari yakiwa na abria. Gari limeunganishwa nyaya. Stendi zote zinapojengwa kuwekwa miundombinu ya kuzima moto na vibanda vya biashara kuacha nafasi kati ya kibanda kimoja na kingine.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara, baadhi ya Maafisa kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Mara, Taasisi za LATRA, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wadau wa usafirishaji.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Mara aunda Kamati kuchunguza ratiba za mabasi madogo

    October 27, 2025
  • Mtambi alipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mara

    October 27, 2025
  • Wananchi Mara wahimizwa kupiga kura kwa amani na utulivu

    October 25, 2025
  • Mtambi awataka wakulima Bunda na Musoma kuchangamkia fursa ya kilimo cha choroko

    October 24, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa