• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtanda ataka ubunifu na kujiongeza Sekta ya Elimu

Posted on: December 19th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mohamed Mtanda leo amefungua kikao cha tathmini ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Mara kinachofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Bunda na kuwataka walimu na wasimamizi wa elimu kuongeza ubunifu na kujiongeza katika utendaji wao wa kazi.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho, Mhe. Mtanda amewataka wasimamizi wa Elimu wa ngazi mbalimbali kufanya ubunifu unaochochea mabadiliko chanya kwa walimu na wanafunzi wanaowasimamia na kuacha alama chanya katika utendaji wao.

“Sio lazima mtu uwe na cheo kikubwa ndio ufanye mabadiliko, unaweza kuwa huna cheo lakini kwa namna unavyochapa kazi na kuongeza ubunifu unaweza kuleta mabadiliko makubwa katika eneo lako kuliko hata mtu mwenye madaraka makubwa ambaye hana ubunifu” amesema Mhe. Mtanda.

Mkuu wa Mkoa pia amewataka Walimu kujiendeleza kimasomo pamoja na kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika maeneo yao ya kazi.

Mhe. Mtanda amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri ambao hawajakamilisha ujenzi wa shule mpya na kuzisajiri kufanyakazi usiku na mchana na kuhakikisha wanasajiri Shule hizo kabla ya tarehe 22 Desemba, 2023 ili ziweze kuanza kuchukua wanafunzi Januari, 2024.

Aidha, amewataka Wakurugenzi, Wasimamizi wa Elimu ngazi mbalimbali kuwasikiliza walimu na kujitahidi kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili ambazo utatuzi wake  upo katika ngazi yao na hauhitaji fedha.

Mhe. Mtanda amewataka wasimamizi wa Elimu kuweka malengo katika utekelezaji wa majukumu yao na katika maisha yao binafsi na kuisemea vizuri  Serikali kwa mambo mazuri inayoyafanya kwa wananchi wa Mkoa wa Mara.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu na Mafunzo Bwana Makwasa Bulenga amewapongeza wasimamizi wa elimu na walimu wa Mkoa wa Mara kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika kufundisha wanafunzi na kuwasimamia walimu.

Bwana Bulenga ameeleza kuwa mwaka  2022 Mkoa ulipanga kufaulisha kwa asiliamia 100 kwa mitihani ya Taifa ya Kidato cha Sita na mwaka 2023 Mkoa umefaulisha kwa asilimia 100 ukiwa na daraja la nne kwa mwanafunzi mmoja tu na kuongeza kuwa matokeo ya mitihani mingine bado hayajatoka lakini anamatumaini kwa kazi iliyofanyika Mkoa wa Mara utafanya vizuri.

Hata hivyo, Bwana Bulenga amesema kwa upande wa mitihani ya kidato cha nne, pili, darasa la saba na darasa la nne bado juhudi zaidi zinahitajika katika kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya kitaifa ya madarasa hayo.  

“Kwa umoja wetu tumepiga hatua kubwa sana katika maendeleo ya elimu ya Mkoa wa Mara japo kuna maboresho zaidi yanahitajika hususan katika shule za msingi na kidato cha kwanza hadi cha nne” amesema Bwana Bulenga.

Bwana Bulenga ameeleza kuwa pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika Mkoa wa Mara kwa mwaka huu, bado Mkoa una upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya Sayansi jambo ambalo amesema linaathiri ufundishaji wa wanafunzi katika masomo hayo.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa shule mpya, Bwana Bulenga amesema tayari baadhi ya Halmashauri zimeshakamilisha ujenzi wa shule mpya na kuzisajiri huku baadhi ya Halmashauri zikiendelea na ukamilishaji wa shule hizo.

Kwa upande wake Bwana Edigga Sibora Mkuu wa Shule ya Sekondari Sazira, Halmashauri ya Mji wa Bunda amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kufungua kikao hicho cha tathmini na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yalitotolewa.

“Sisi tunaahidi hatutakuangusha katika kuleta mabadiliko katika maeneo yetu ya kazi na katika maisha yetu sisi wenyewe” amesema Bwana Sibora.

 Kikao hicho cha siku mbili ambacho Mwenyekiti wake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Msalika Robert Makungu,  kimehudhuliwa na Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wasimamizi wa Elimu ngazi ya Mkoa, Halmashauri, wadau wa elimu na baadhi ya walimu wakuu na wakuu wa shule.

Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • Waongozeni wanafunzi kufikia ndoto zao- Kusaya

    May 29, 2025
  • Kamati za Maafa Mkoa wa Mara zajengewa Uwezo

    May 26, 2025
  • Kikwete achangisha milioni 200 za ujenzi wa kanisa Mara

    May 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa