• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi awataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wawekezaji

Posted on: January 1st, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 01 Januari, 2026 amezindua kituo cha Mafuta cha GBP katika eneo la Makutano ya Juu, Wilaya ya Butiama na kuwataka wananchi wa Mkoa wa Mara kutoa ushirikiano kwa wawekezaji waliopo katika maeneo yao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho Mhe. Mtambi amesema wawekezaji wanafaida kubwa kwa jamii inayowazunguka ikiwa ni pamoja na kupata bidhaa na `huduma kjirani na maeneo yao jambo ambalo amesema bila uwekezaji huo wangefuata bidhaa au huduma hizo mbali na kuwaongezea gharama.

“Kwa mfano kituo hiki cha mafuta kisingekuwepo mngelazimika kufuata mafuta mbali na hapa jambo ambalo lingewaongezea gharama, lakini pia kimetoa ajira kwa vijana wa Mkoa wa Mara na Butiama kisingekuwepo na ajira zisingekuwepo” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amewakemea wanaoharibu mali za wawekezaji kwa kuwa faida ya uwekezaji wowote ule inaenda hadi kwa jamii inayozunguka uwekezaji huo na kuwaletea manufaa jamii husika na hivyo ni muhimu wananchi kulinda uwekezaji wa Serikali na kampuni binafsi uliopo katika maeneo yao kwa kuwa unamanufaa kwao.  

Mkuu wa Mkoa amewahamasisha wananchi kukumbuka kuwa suala la kuilinda nchi ya Tanzania ni jukumu lao kwani suala la ulinzi wa nchi ni la wananchi wote na vyombo vya ulinzi vinajukumu la kutoa uongozi na utaalamu kuhusiana na namna bora ya kulinda nchi.

Kanali Mtambi amewataka wananchi na hususan Maafisa Usafirishaji kuacha kutumika na watu wabaya kuharibu miundombinu iliyojengwa katika maeneo yao kwani uwekezaji huo umefanyika kwa manufaa yao kwa kuwa Serikali inahakikisha katika uwekezaji wowote unaofanyika, mwananchi anafaidika.

Mhe. Mtambi amesema uwekezaji wa Kampuni ya GBP hapa nchini unatokana na  sheria na sera nzuri za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza Tanzania.

Mhe. Mtambi ameipongeza Kampuni ya GBP kwa kuwekeza katika Mkoa wa Mara na kuwahamasisha wawekezaji wengine kuwekeza katika fursa mbalimbali zilizopo katika Mkoa wa Mara katika sekta za madini, utalii, usafirishaji na huduma mbalimbali.  

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Mara amewapongeza viongozi, wadau na wananchi wa Wilaya ya Butiama kwa amani na utulivu waliyoionyesha wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 jambo ambalo amesema ni mfano wa kuigwa.

“Wakati tunahangaika kuhakikisha amani na utulivu vipo katika Mkoa wa Mara, wananchi wa Wilaya ya Butiama walikuwa wakiendelea na shughuli zao za uzalishaji mali na kuonyesha ukomavu wa kisiasa wa kuigwa na wapenda amani wote hapa nchini” amesema Mhe. Mtambi.

Akizungumza wakaati wa kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Thecla Mkuchika ameipongeza Kampuni ya GBP kuwekeza katika Wilaya ya Butiama na kuwahakikishia kuwa Butiama ni sehemu sahihi ya uwekezaji.

Mhe. Mkuchika amewataka wananchi wa Wilaya ya Butiama na Mkoa wa Mara kwa ujumla kutumia kituo hicho cha mafuta katika kupata huduma mbalimbali za kisasa na mafuta yenye ubora wa uhakika.  

Kwa upande wake, Afisa Ufuatiliaji wa Kampuni ya GBP Tanzania Ndugu Dawood Sadikot amesema kambpuni hiyo ina uzoefu wa uuzaji wa mafuta hapa nchini kwa zaidi ya miaka 25 na imeajiri ajira za moja kwa moja watumishi zaidi ya 1,000.

“Ujenzi wa kituo hiki ni mwendelezo wa biashara zetu nchini Tanzania na tunaishukuru Serikali kwa kuweka mazingira mazingira mazuri ya uwekezaji yanayowawezesha kuwekeza na kusaidia katika ujenzi wa Tanzania” amesema Ndugu Sadikot.

Ndugu Sadikot amesema kampuni hiyo inajivunia wafanyakazi wake kwa kufanya kazi kwa nidhamu, uadilifu, weledi na kutoa huduma bora kwa wateja hapa nchini na kuwataka wananchi wa Wilaya ya Butiama kukitumia kituo hicho kupata huduma za kisasa.

 Hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mafuta cha GBP imehudhuliwa pia na Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Butiama, Mbunge wa Jimbo la Butiama Dkt. Charles Wilson Mahera, Maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na Halmashauri ya Wilaya ya Butiama.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mtambi awataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wawekezaji

    January 01, 2026
  • Nyansaho ateta na Wazee wa Mara

    December 24, 2025
  • Mtambi: Mara imejipanga kuhakikisha usalama wakati wa sikukuu

    December 24, 2025
  • Serikali yaipongeza Mara kwa mabadiliko

    December 24, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa