• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi ashsiriki mapokezi ya Chapo

Posted on: June 12th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo amewaongoza wananchi wa Mkoa wa Mara katika mapokezi ya Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO na Mgombea Uraisi wa Nchi ya Msumbiji Mhe. Daniel Francisco Chapo ambaye ametembelea makazi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika eneo la Mwitongo, Butiama.

Akizungumza katika mapokezi hayo, Mhe. Mtambi amemshukuru amesmhukuru Mhe. Chapo kwa kuamua kutembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa na kuwashukuru viongozi na wananchi waliojitokeza kushiriki mapokezi hayo.  

Akiwa Butiama Mhe. Chapo amesalimiana na wananchi wa Butiama waliojitokeza kumlaki, amezungumza na wanafamilia ya Mwalimu Nyerere wakiongozwa na mtoto wa Mwalimu Nyerere Madaraka Nyerere, viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) waliokuja kumlaki.  

Mhe. Chapo ametembelea kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuweka shada la maua kabla ya kuwasalimia mamia ya wananchi wa Butiama waliojitokeza kumpokea katika Uwanja wa Mwenge Butiama.  

Viongozi walioshiriki mapokezi hayo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Mhe. John Mongela, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Bwana Patrick Chandi na viongozi wengine wa CCM Taifa, Mkoa na Wilaya.  

Viongozi wengine waliokuwepo katika mapokezi hayo ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Butiama Mhe. Jumanne Sagini na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Moses Kaegele, wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Mkoa na Wilaya ya Butiama.

Katika mapokezi hayo,Bwana Madaraka Nyerere amempatia Mhe. Chapo fimbo inayofanana na fimbo ambayo Baba wa Taifa alikuwa anatembea nayo wakati wa uhai wake ambayo alisema kwa Kizanaki fimbo hiyo ilikuwa ni ishara ya uongozi thabiti.   

Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kusaya awataka wahanga kutumia misaada kuboresha maisha

    May 19, 2025
  • BASATA yaijengea uwezo Mkoa wa Mara

    May 15, 2025
  • Mara kutumia fursa zilizopo kuboresha sanaa kwa vijana

    May 15, 2025
  • RC aipongeza Musoma ushindi wa ubora wa huduma za afya Kitaifa

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa