• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi aiomba Wizara ya Maji kuongeza uwekezaji katika miradi ya maji Mara

Posted on: January 5th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 05 Januari, 2026 amempokea na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Kundo Mathew na kuiomba Wizara ya Maji kuwekeza katika miradi zaidi ya maji katika baadhi ya maeneo ya Wilaya za Musoma, Serengeti, Rorya, Tarime na Bunda.

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Mhe. Mtambi amesema kwa sasa upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Mara ni mzuri lakini kuna baadhi ya vijiji katika wilaya hizo havijafikiwa na mtandao wa miradi ya maji na hivyo kuyafanya maeneo hayo kukosa maji.

“Hali ya upatikanaji wa maji katika maeneo mengi ya Mkoa wa Mara ni nzuri lakini kuna baadhi ya maeneo katika Wilaya za Musoma, Serengeti, Rorya, Tarime na Bunda wananchi hawana maji safi na salama ya uhakika na baadhi ya maeneo haya miradi mikubwa imeanza kutekelezwa lakini haijakamilika” amesema Mhe. Mtambi.

Kanali Mtambi ameiomba Serikali kukamilisha kwa wakati miradi ya kimkakati ya maji itakayohudumia wananchi katika wilaya za Rorya, Tarime na mradi wa maji wa Serengeti ili wananchi wa Wilaya hizo waweze kupata maji ya uhakika.

Mhe. Mtambi amesema wananchi wanaokosa maji ya uhakika, wakipata maji itawasaidia kutumia muda wao katika shughuli za kiuchumi na kuboresha upatikanaji wa maji ambayo amesema ni huduma muhimu katika maisha ya wananchi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maji Mhe. Kundo Mathew amesema kwa sasa Wizara ya Maji ina mkakati madhubuti wa kuboresha upatikanaji wa huduma za maji katika maeneo yote hapa nchini ambapo viongozi na wataalamu wanafanya ziara kwa lengo la kubaini mahitaji halisi ya wananchi ili kubuni miradi itakayotatua tatizo hilo.

Mhe. Mathew amesema baada ya ziara hizo Wizara itapanga miradi ya maji kulingana na mahitaji halisi ya wananchi katika Mikoa yote hapa nchini na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha miradi ya mikubwa ya maji inayotekelezwa katika Mkoa wa Mara itakamilika kwa wakati ili ianze kutoa huduma kwa wananchi. 

Mhe. Mathew amezitaka Mamlaka zote za maji nchini kufanya mapitio ya vyanzo vya maji na kuangalia hali yake kwa ujumla pamoja na kubuni vyanzo mbadala vya maji pale ambapo vyanzo vilivyopo havitoshelezi mahitaji ya sasa na yanayotarajiwa ya wananchi.

Mhe. Mathew amewataka watendaji wa sekta ya maji kuacha kufanya kazi kwa dharura na badala yake wafanyekazi kwa mpangilio endelevu na sahihi ili kuongeza ufanisi katika sekta ya maji nchini.

Katika mapokezi hayo Mhe. Mathew ameambatana na maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, taasisi za RUWASA, Ofisi za Bonde la Ziwa Victoria Mkoa wa Mara, Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA), Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Mji wa Bunda (BUWSSA), na Mamlaka ya Maji Mgango- Kiabakari.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mara yaweka mikakati kukomesha ukeketaji

    January 06, 2026
  • Mara haitamvumilia atakayeyumbisha sekta ya elimu: Mtambi

    January 06, 2026
  • Kutupa taka ovyo Mara ni hujuma za kiuchumi: Mtambi

    January 06, 2026
  • Mara yaazimia kufuatilia utekelezaji wa miradi ya barabara

    January 06, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa