• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mara yapokea mbio za Mwenge wa Uhuru

Posted on: August 15th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya leo tarehe 15 Agosti, 2025 amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Ndugu Prisca Joseph Kayombo katika uwanja wa Shule ya Msingi Balili, Kata ya Nyamakokoto, Halmashauri ya Mji wa Bunda, Wilaya ya Bunda.

Akizungumza wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru, Ndugu Kusaya amewahamasisha wananchi wa Mkoa wa Mara kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ili kutumia haki yao ya kikatiba na kidemokrasia kuwachagua viongozi mbalimbali watakaoliongoza Taifa kwa miaka mitano ijayo.

Ndugu Kusaya amesema Mkoa wa Mara umejipanga vizuri kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na mpaka sasa mafunzo kwa ajili ya wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo wamepatiwa mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi na mafunzo ya wasimamizi ngazi ya kata yanaendelea.

“Kwa kuzingatia kuwa zoezi la uchaguzi ni shirikishi, vikao vya wadau mbalimbali wa uchaguzi katika Mkoa wa Mara vimefanyika na vitaendelea kufanyika” amesema Bwana Kusaya  kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba, 2025.

Aidha, Bwana Kusaya amewataka wananchi kutunza  kadi ya mpiga kura, kushiriki katika mikutano ya kampeni ili kuwasiliza wagombea, kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, kuheshimu, kuzingatia katiba, sheria, kanuni na maelekezo yatakayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, kuepuka vitendo vya rushwa na kushirikiana na viongozi watakaochaguliwa.

Ndugu Kusaya amesema Mwenge ukiwa katika Mkoa wa Mara utakimbizwa katika umbali wa kilomita 1,123 na utatembelea miradi 68 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 26,547,598,285.42 katika sekta za elimu, afya, maji, ujenzi, kilimo, mifugo, mazingira, ustawi wa jamii, viwanda na biashara.

Ndugu Kusaya amesema Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Mkoa wa Mara utapita nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwitongo, Butiama na ukiwa hapo utapata nafasi ya kuwasha Mwenge wa Mwitongo.

“Ndugu kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa ukiwa Mwitongo utapata nafasi ya kuzuru na kuweka mashada ya maua katika kaburi la Baba wa Taifa na kutembelea makumbusho ya Baba wa Taifa na kupata historia ya Baba wa Taifa” amesema Ndugu Kusaya.

Ndugu Kusaya amechukua fursa hiyo kuwakaribisha viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mara na Simiyu kushiriki tukio la kuwashwa kwa Mwenge wa Mwitongo siku ya Jumatatu tarehe 18 Agosti, 2025 kuanzia saa sita mchana.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Ndugu Kayombo amesema Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Mkoa wa Simiyu umekimbizwa katika Halmashauri sita kwa siku sita na kuwapongeza wakimbiza Mwenge wa Uhuru kwa kazi kubwa waliyoifanya katika Mkoa wa Simiyu.

Baada ya mapokezi hayo, Bwana Kusaya amekabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda Ndugu Salum Khalfan Mtelala kwa ajili ya kuendelea na mbio zake katika Halmashauri ya Mji wa Bunda na mkesha wa Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kufanyika Shule ya Msingi Miembeni.

Hafla ya mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru zimehudhuriwa na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara, Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mara, Viongozi wa Vyama vya Siasa wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Mhe. Chandi Patrick Marwa, Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa wa Mara, viongozi, watumishi, wadau na wananchi mbalimbali kutoka mikoa ya Mara na Simiyu.  

 Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu ni “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu” na Mwenge utakimbizwa katika Halmashauri zote tisa hadi tarehe 23 Agosti, 2025 na kukabidhiwa katika Mkoa wa Mwanza tarehe 24 Agosti, 2025 kuendelea na mbio zake.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Maambukizi ya UKIMWI katika Wilaya ya Bunda yamepungua

    August 16, 2025
  • Mara yapokea mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 15, 2025
  • Kusaya ateta na viongozi wa Bodi ya Mkonge

    August 14, 2025
  • Mwenge wa Uhuru kupitia miradi ya bilioni 26.6 Mara

    August 13, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa