• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Makungu awataka Walimu Wakuu Mara kuboresha Elimu

Posted on: October 2nd, 2023

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Msalika Robert Makungu leo amefungua rasmi mafunzo ya kuwajengea uwezo Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kutoka Halmashauri tano za Mkoa wa Mara yanayofanyika katika Chuo cha Ualimu Bunda na kuwataka Walimu Wakuu kusaidia kuboresha elimu ya msingi hapa nchini.

Bwana Makungu amewataka Walimu Wakuu kutumia mafunzo haya waliyopewa na Mradi wa BOOST  kuboresha utendaji, uongozi  na usimamizi wao katika miradi ya elimu na kuacha kufanyakazi kwa mazoea.

“Uongozi sio kazi rahisi sana, ukiiona rahisi basi wewe utakuwa hufanyi kinachotakiwa kufanyika, uongozi ni dhamana na mafunzo haya yawasaidie katika kuboresha utendaji, usimamizi na uongozi wenu katika shule zenu, tuone mabadiliko” amesema Bwana Makungu.

Bwana Makungu ameeleza kuwa kama Walimu Wakuu wakitimiza wajibu wao vizuri, maboresho katika elimu yataonekana kwa wazi na watu watajua kuwa shule zinazongozwa na viongozi walioiva vizuri na kusimamia ufundishaji, watumishi, rasilimali na miradi ya maendeleo.

Kwa mujibu wa Bwana Makungu, Serikali imeboresha miundombinu, idadi ya walimu na watumishi, mishahara na madai mbalimbali yamelipwa vizuri kinachohitajika kikubwa ni Walimu Wakuu wenye kujituma na kuonyesha mfano katika kusimamia ili kama Taifa tuweze kunufaika na uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu.

Aidha, amewataka Walimu Wakuu kuwashirikisha kuhusu miradi, mipango na bajeti watumishi wote walio chini yao ili kupata uungwaji mkono katika utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyopo katika Shule za Msingi na kuacha kuwa na makundi ya watumishi katika shule hizo.  

Bwana Makungu amewataka Walimu Wakuu kutoa taarifa kwa viongozi wa Halmashauri na Mkoa wanapoona wanaingiliwa katika manunuzi ya vifaa na utendaji wao wa kila siku na viongozi au watu wengine nje ya mfumo wa elimu.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu Bibi Judith Mrimi amesema amesema mafunzo hayo ni utekelezaji wa afua namba nne ya mradi wa BOOST ambayo inalenga kuboresha uongozi na usimamizi katika elimu.

Bibi Mrimi amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuboresha uongozi, usimamizi na uendeshaji wa Shule za Msingi katika Mkoa wa Mara na kuwaomba walimu kujifunza na baadaye kuyafanyia kazi mafunzo waliyopewa.

Mafunzo hayo kwa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi yametolewa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia Mradi wa BOOST na kutolewa na wakufunzi kutoka Chuo cha Uongozi wa Elimu, Bagamoyo (ADEM) na Maafisa Elimu Taaluma wa Halmashauri zilizohusika.

Mafunzo hayo ya siku tatu kwa awamu ya kwanza yamewahusisha Walimu Wakuu 415 kutoka  Shule za Msingi kutoka Halmashauri za Mji wa Bunda, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na Manispaa ya Musoma.

Kwa awamu ya pili mafunzo kama hayo yatafanyika katika Mji wa Tarime na kuwahusisha walimu Wakuu kutoka Shule za Msingi za Halmashauri za Tarime Mji, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na Halmashauri ya Wilaya ya Rorya.

 Ufunguzi wa mafunzo hayo umehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda Bwana Salum Mtelela, Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mara Bwana Adam Janga,  Mkuu wa Chuo cha Ualimu Bunda, wakufunzi kutoka ADEM na Maafisa Elimu Taaluma wa Halmashauri zilizohusika.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wananchi Rorya wahimizwa kutumia nishati safi ya kupikia

    August 19, 2025
  • Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa awasha Mwenge wa Mwitongo kwa mara ya 61

    August 18, 2025
  • Mwenge wakagua miradi ya bilioni 6 Musoma

    August 18, 2025
  • Maambukizi ya UKIMWI katika Wilaya ya Bunda yamepungua

    August 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa