• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Makabidhiano ya Mali za Ushirika yafanyika Mara

Posted on: December 14th, 2022

Makabidhiano ya mali za uliokuwa ushirika wa Mara Cooperative Union 1994 Ltd kwa vyama vya ushirika vya mazao ya pamba na kahawa yamefanyika leo katika Kiwanda cha Kuchambua Pamba na Mafuta ya Pamba cha Mgango  katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mufilisi wa Ushirika huo Bwana Juma Shaaban Mrisho ameeleza kuwa mali zinazokabidhiwa ni pamoja na viwanda vinne vya mazao vyenye thamani ya shilingi bilioni 5.2 na madeni ya zaidi ya shilingi bilioni 10.5.

“Madeni haya yanajumuisha madeni ya chama cha Ushirika cha Mara Cooperative Unioni 1994 Ltd ikiwemo mkopo kutoka Benki ya Biashara (NBC), madai ya watumishi na madeni kwa taasisi mbalimbali na madeni yaliyotokana na shughuli za ufilisi.

Bwana Mrisho ameeleza kuwa mali nyingine za ushirika huo ni Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Songe iliyopo katika Manispaa ya Musoma yenye thamani ya shilingi milioni 550 ambayo Serikali iliichukua na kuanzisha Shule ya Sekondari ya Wasichana.

Aidha, Bwana Mrisho ameeleza kuwa katika kipindi chote walichofanya kazi ya ufilisi wa ushirika huo tangu mwaka 1996 walifanikiwa kukusanya shilingi bilioni 1.9 ambazo zilitumika katika shughuli za ufilisi wa ushirika huo kuanzia wakati huo hadi tarehe 12 Desemba, 2022.

“Kutokana na kuchelewa zoezi la makabidhiano, zoezi la ufilisi lilikuwa likizalisha madeni kila mwaka, viwanda kuchakaa na kupungua thamani na wananchi kuvamia maeneo ya viwanda vinavyomilikiwa na ushirika huo ndio baadhi ya changamoto tulizokabiliana nazo” alisema Bwana Mrisho.

Kwa upande wake, Mrajisi wa Ushirika kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege ameeleza kuwa mgawanyo wa mali na madeni kwa vyama hivyo umetegemea zaidi mazao wanayoshughulika nayo.

Ameeleza kuwa katika mgawanyo huo, WAMACU wanapata Kiwanda cha Kawaha cha Tarime, ardhi ya kiwanda hicho na asilimia 20 ya deni lote lililobakia wakati PMCU inapata viwanda vya pamba vya Mugango (Musoma), Kibara  na Rushashi (Bunda) pamoja na ardhi ya viwanda hivyo na mali zilizomo na madeni asilimia 80.

Aidha, Bwana Ndiege ameeleza kuwa madeni hayo bado yanaendelea kuhakikiwa uhalali wake na Ofisi ya Mrajisi utasimamia kuhakikisha madeni yote yanalipwa kwa mujibu wa sheria.  

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Gambaless Timotheo ameeleza kuwa urejeshaji wa mali hizo za ushirika utasaidia kuchochea ukuaji wa kilimo cha mazao ya pamba na kahawa katika Mkoa wa Mara.

“Ni matumaini yangu mtakuja na mkakati madhubuti wa kuendeleza viwanda hivi na kuzitunza mali za ushirika mlizokabidhiwa leo kwa manufaa ya wanaushirika wote wa Mkoa wa Mara” alisema Bwana Timotheo.  

Bwana Timotheo ameipongeza Ofisi ya Mrajisi na Mufilisi kwa kusimamia zoezi hilo vizuri na kuhakikisha vyama hivyo vinapata mali zao zikiwa salama na makabidhiano yanafanyika kwa amani.

Wakati huo huo, Bwana Timotheo amevipongeza  WAMACU na PMCU kwa kuonyesha tija katika kipindi kifupi na kuwezesha kuaminiwa na Serikali na  kuvitaka vyama hivyo kuvirejesha viwanda vyote katika uzalishaji ili wananchi wapate soko la kuuzia mazao yao kwa urahisi.

Bwana Timotheo ameeleza kuwa Mkoa wa Mara katika msimu huu wa kilimo umepanga kupata tani 25,000 za kahawa na tani 80,000 za pamba lakini anatarajia baada ya makabidhiano hayo na viwanda kuanza kufanyakazi kutakuwa na mapinduzi ya kilimo cha mazao hayo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Kahawa Mkoa wa Mara (WAMACU LTD) Bwana David Mwita Hechei ameishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kuzitoa mali za ----kwa ushirika wao na kuahidi kuzitumia mali hizo kama mtaji wa kuendeleza shughuli za ushirika.  

Bwana Heichei ameiomba Serikali katika ngazi zote kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyama hivi vya ushirika vilivyokabidhiwa mali na madeni kuhakikisha vinaendelea kufanya shughuli zake kwa maendeleo ya wanaushirika.

Aidha, ameiomba serikali kurejesha mali za vyama vya msingi vya ushirika zilizokabidhiwa kwa Serikali za Vijiji ili vyama vya ushirika vya msingi viweze kupata mali hizo ili kuviendeleza.  

Bwana Heichei ameiomba Serikali kuendelea na uhakiki wa madeni waliyokabidhiwa ili vyama hivyo vilipe madeni yake halali tu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Pamba Mara Cooperative Union (PMCU) Bwana Daudi Kisingi Iramba ameeleza kuwa leo ni siku ya furaha sana kwa kuwa baada ya miaka 26 mali za wanaushirika zimerudi kwa wanaushirika wa Mkoa wa Mara.

Bwana Iramba ameahidi kuandaa mpangokazi  wa vyama vyao vya ushirika na kuukamilisha kabla ya tarehe 1 Januari, 2023 kama walivyoelekezwa na kuuwasilisha Ofisi ya Mrajisi kwa hatua zaidi.

Aidha, Bwana Iramba ameahidi kuwa viwanda walivyokabidhiwa vitaanza kufanyakazi mara moja kwa maendeleo ya wanaushirika na wananchi wote wa Mkoa wa Mara.

Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kusaya awataka wahanga kutumia misaada kuboresha maisha

    May 19, 2025
  • BASATA yaijengea uwezo Mkoa wa Mara

    May 15, 2025
  • Mara kutumia fursa zilizopo kuboresha sanaa kwa vijana

    May 15, 2025
  • RC aipongeza Musoma ushindi wa ubora wa huduma za afya Kitaifa

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa