• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Maambukizi ya UKIMWI katika Wilaya ya Bunda yamepungua

Posted on: August 16th, 2025

Adeladius Makwega BUNDA MARA

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Aswege Enock Kaminyonge tarehe 15 Agosti, 2025 amesema kiwango cha maambukizi ya virusi vya HIV na UKIMWI katika Wilaya ya Bunda kimepungua kutoka asilimia 2.4 hadi asilimia 1.5 kutokana na jitahada za pamoja kwa ushirikiano thabiti, baina wa wananchi, wadau na Serikali ya inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mhe. Kaminyonge akizungumzia takwimu za upimaji wa magonjwa amesisitiza kuwa zoezi la upimaji wa VVU na UKIMWI kwa hiari katika Mbio za Mwenge wa uhuru linafanyika, hivyo basi mara baada ya Mwenge kwenda Halmashauri nyingine Halmashauri ya Mji wa Bunda itakuwa na takwimu juu ya muitikio wa wananchi katika zoezi hili.

Akizungumza akizungumza kwa nyakati tofauti, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu Ussi amesema ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa kutekeleza miradi yenye ubora kwa kuzingatia vigezo vya Serikali na kuwataka wananchi wa Wilaya ya Bunda kutembea kifua mbele.

“Huo ubora wa miradi yenu, ndiyo shabaha ya serikali yetu, jamani endeleeni kufanya kazi kwa bidii” amesema Bwana Ussi.

Ndugu Ussi aamesisitiza suala la afya kwa kila Mtanzania kujitahidi kufuata kanuni na maelekezo ya wataalamu wa afya ili baada ya kuwa na afya bora wananchi wajikite kufanya kazi zao za maendeleo bila kikwazo chochote.

“Tujikinge na VVU na UKIMWI na ndiyo maana kumekuwa na semina na mafunzo kadhaa kwa shule 37 na pia kutoa elimu kwa kutumia video, senema na vipeperushi, huku kwa sasa kukiwa na mabanda ya kutoa ushauri wa afya ikiwamo upimaji magonjwa mbalimbali ”amesema Ndugu Ussi.

Akisoma Risala ya Utii Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katibu Tawala Wilaya ya Bunda Ndugu Salum Mtelela mbele ya Mwenge wa Uhuru, mara baada ya kufungua miradi 8 na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025, Ndugu Ismail Ali Ussi baada ya kuwasili katika Halmashauri hiyo.

Mbio hizo zilianza kukimbizwa mara baada ya Mwenge wa Uhuru kupokelewa na Katibu Tawala Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Msabila Kusaya mapema leo Halmashauri ya Mji wa Bunda ukitokea Mkoani Simiyu.

Awali katika makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru baina ya Mkoa wa Mara na Simiyu, Katibu Tawala Mkoa wa Mara Ndugu Kusaya amewakaribisha wakimbiza Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Mara maana Mara ndipo alipozaliwa muasisi wa Mwenge wa Uhuru na Baba wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Katika Halmashauri ya Mji wa Bunda Miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tatu katika sekta za elimu, afya, barabara, maji, mapambano dhidi ya rushwa na kituo cha mafuta cha NM imefunguliwa.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Maambukizi ya UKIMWI katika Wilaya ya Bunda yamepungua

    August 16, 2025
  • Mara yapokea mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 15, 2025
  • Kusaya ateta na viongozi wa Bodi ya Mkonge

    August 14, 2025
  • Mwenge wa Uhuru kupitia miradi ya bilioni 26.6 Mara

    August 13, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa