• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Ianzishwe Mamlaka ya Usimamizi wa Ziwa Victoria

Posted on: December 24th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 22 Disemba, 2025 amempokea Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mhe. Ng’wasi Damas Kamani na ameiomba Serikali ianzishe kwa haraka Mamlaka ya Usimamizi wa Ziwa Victoria.

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Mhe. Mtambi amesema Mamlaka hiyo itasimamia uhifadhi na udhibiti wa shughuli zote zinazofanyika ndani ya Ziwa Victoria na hivyo ziwa hilo kupata usimamizi endelevu.

“Kwa sasa kila taasisi inafanya udhibiti na usimamizi kivyake na hamna taasisi moja inayowaunganisha na kuziratibu shughuli za taasisi nyingine za Serikali ndani ya Ziwa Victoria” amesema Mhe. Mtambi na kuongeza kuwa Mamlaka hiyo itaratibu sheria mbalimbali zinazolenga kulihifadhi Ziwa Victoria kwa kuzisimamia kwa ukaribu.

Mhe. Mtambi amesema kwa sasa changamoto kubwa ya ziwa hilo ni uhalifu unaofanyika katika ziwa, uvuvi haramu, magugu maji, uhifadhi wa mazingira ya Ziwa na kuongeza kuwa cchangamoto hizo zinaweza kupunguzwa kwa kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo.

Kanali Mtambi amesema kwa kuwa Mamlaka hiyo itasimamia sheria na kukusanya maduhuli yanayotokana na Ziwa Victoria, Serikali haitapata gharama ya ziada ya kuiendesha mamlaka hiyo na badala yake Mamlaka hiyo inaweza kuchangia fedha katika Mfuko Mkuu wa Serikali kama zilivyo Hifadhi za Taifa hapa nchini.

Wakati huo huo, Mhe. Mtambi amemuomba Mhe. Waziri kufuatilia mradi wa utengeneza wa chakula cha samaki na uzalishaji wa vifaranga vya samaki katika Kituo cha TAFIRI kilichopo Sota, Wilaya ya Rorya ili wafugaji wa samaki katika vizimba katika Mkoa wa Mara waweze kupata chakula cha samaki kwa urahisi.

“Kwa sasa wafugaji wa samaki katika vizimba wanapata chakula kutoka mikoa na nchi jirani kwa gharama kubwa lakini kiwanda hiki kikikamilika kitawawezesha wafugaji kupata chakula kwa urahisi” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amesema Mkoa wa Mara umewahamasisha sana wananchi kufuga samaki kwa njia ya vizimba hata hivyo wafugaji walioitikia wito huo wanakutana na changamoto ya bei za chakula cha samaki jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za Serikali kuhamasisha uzalishaji wa samaki kwa njia ya vizimba.

Akizungumza katika mapokezi hayo, Mhe. Kakurwa amesema suala la kuanzisha taasisi ya kudhibiti shughuli za kwenye maziwa na mito mikubwa Serikali imeliona na limo katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2025/2030 na Wizara imeanza kulifanyia kazi na tayari andiko la kuanzisha mamlaka hiyo lipo tayari linasubiri kupitishwa na vikao mbalimbali.

Aidha, Mhe. Kakurwa ameiagiza TAFIRI kuwasilisha taarifa za mradi wa kutengeneza chakula cha samaki Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kabla hajahitimisha ziara yake ili maamuzi yaweze kuchukuliwa kwa haraka.

Mhe. Kakurwa ameahidi ushirikiano baina yake na Mikoa na Serikali za Mitaa ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara hiyo katika kuimarisha sekta za mifugo na uvuvi.

 Katika ziara hiyo, Mhe. Kakurwa ameambatana na Naibu Waziri na Maafisa mbalimbali kutoka Wizarani na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya wakati na baada ya uchaguzi yaingia Mara

    January 08, 2026
  • Mara yaweka mikakati kukomesha ukeketaji

    January 06, 2026
  • Mara haitamvumilia atakayeyumbisha sekta ya elimu: Mtambi

    January 06, 2026
  • Kutupa taka ovyo Mara ni hujuma za kiuchumi: Mtambi

    January 06, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa