Friday 27th, December 2024
@Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara
Mkoa wa Mara unatarajia kuandikisha wananchi Milioni moja na laki tatu kwa muda wa miezi mitatu. Mpango huu wa Mkoa ni kutokana Mkoa wa Mara umepakana na nchi jirani ya Kenya. Mkoa umeona kuna kila sababu ya kuhakikisha kila mwananchi wa Mkoa wa Mara anapata Kitambulisho cha Taifa ili kuweza kutambuana na hatimaye kuweza kupambana na waamiaji haramu na vitendo vya uharifu.
Zoezi hili linatarajia kuanza tarehe 22/11/2107 na kumalizika tarehe 12/03/2017. Zoezi hili litaendeshwa Wilaya zote sita za Mkoa wa Mara. Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe.Adam Kighoma Malima anaomba wananchi wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha ili waweze kupata vitambulisho vya Taifa.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa