Friday 27th, December 2024
@Uwanja wa Sokoine Mugumu-Serengeti
Maadhimisho ya nane ya Mara day ni mwendelezo wa kampeni juu ya Uhifadhi wa bonde la Mto Mara. Maadhimisho haya yanafanyika kwa zamu baina ya nchi mbili Tanzania na Kenya. Katika maadhimisho haya shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwa ni pamoja na Uwekaji wa bikoni, Upandaji miti katika bonde la mto Mara, elimu ya lishe , mashindano ya michezo ya riadha na mpira wa miguu pamoja na maonesho ya bidhaa mbalimbali. Maadhimisho haya yatafanyika kuanzia tarehe 12-15/09/2019 katika uwanja wa Sokoine -Mugumu Wilayani Serengeti Mkoa wa Mara. Mgeni rasmi katika maadhimisho haya ni Waziri Mkuu wa Tanzania - Mhe. Kassim M. Majaliwa(Mb).
Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni: '' Mimi Mto Mara, Nitunze Nikutunze.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa