• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Uvuvi


Tanzania inamiliki asilimia 51 ya eneo la Ziwa Victoria ambayo ni sawa na Kilomita za mraba 35, 088. Aidha Mkoa wa Mara unamiliki Kilomita za mraba 9,825 sawa na asilimia 28 ya sehemu ya umiliki wa Tanzania. Wilaya zinazopakana na Ziwa kwa upande wa Mkoa wa Mara ni Bunda, Butiama, Musoma na Rorya. Uwepo wa Ziwa Victoria umechangia sana kutokana na mazao ya samaki kutumika kwa matumizi ya chakula kwa binadamu na mifugo. 

AJIRA ZITOKANAZO NA SEKTA YA UVUVI.

Sekta ya uvuvi inatoa ajira ya moja kwa moja (direct employment) kwa wavuvi na ajira isiyo ya moja kwa moja (indirect employment) kwa wadau wengine. Mwaka 2014 sekta ya uvuvi Mkoa wa Mara imetoa ajira kwa   wavuvi 24,220 hii ni pungufu ya wavuvi 1,158 ikilinganishwa na wavuvi 25,378 mwaka 2012. Upungufu huu pamoja na mambo mengine unatokana na kupungua kwa rasilimali ya sekta ya uvuvi. Aidha kutokana na utafiti wa shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa  (FAO) mvuvi mmoja anatoa ajira kwa watu angalau 4 (kama vile, wachakataji wa samaki, wachuuzi na wafanya biashara ya samaki, wamiliki wa vyombo vya uvuvi, mafundi boti, washona nyavu na wauzaji wa zana za uvuvi, mama lishe n.k.). kwa mantiki hii sekta ilitoa ajira pia kwa wadau wengine wasiopungua  96,880 kwa mwaka 2014.

WASTANI WA UVUNAJI WA SAMAKI

Kwa mwaka 2015/2016  zilivuliwa tani 21,241.139 za samaki wenye thamani ya   Shilingi  96,988,512,313  pesa hizi ni mapato ya wavuvi.

Wamiliki wa viwanda vya samaki (Musoma Fish na Prime Catch) kwa mwaka 2015/2016 wamepata Shilingi 45,793,965,671.87 kutokana na mauzo ya Kilogramu  2,765,753 za samaki na mazao yake nje ya Nchi na kulipa Mrabaha wa Shilingi 834,274,048. Aidha wasafirishaji wadogo wa samaki na mazao yake  walipata jumla yaShilingi 105,214,740 kwa mauzo ya kilo 297,425 za dagaa, furu na unga wa Samaki katika soko la Nchi ya Kenya. Kwa upande wa Serikali kuu na Halmashauri za Wilaya na Manispaa zilipata jumla ya Shilingi 1,910,607,617 kutokana  na ada na tozo mbalimbali za shughuli za uvuvi ( Serikali kuu Tshs. 955,918,403 na Halmashauri Tshs. 954,689,214.

MIALO YA SAMAKI

Kwa mujibu wa sensa ya uvuvi 2014, Mkoa una jumla ya mialo 174 ambapo mialo 172 inasimamiwa na vikundi vya wadau wa uvuvi (BMUs). Mialo yenye vibanda / majengo ya kupokelea samaki ni 17. Aidha, mialo 99 ina huduma za afya (healthy clincs), mialo 131 ina shule za msingi, mialo 30 ina vyoo vya umma, mialo 165 ina huduma za benki , mialo 6 ina huduma ya umeme na mialo 79 inafikika kwa barabara wakati wowote. Sambamba na kutegemea Ziwa Victoria Sekta ya Uvuvi imekuwa ikikua kwa kasi kubwa kwani hadi kufikia Mwezi Desemba 2016, jumla ya mabwawa 319, vizimba 58 na malambo / mabwawa ya asili 72 (malambo 24 ni ya kudumu na yana samaki) yenye samaki aina ya Sato (Oreochromis sp.) na Kambale (Clarius sp).

Mkoa wa Mara umeendelea kusimamia ipasavyo Sera ya uvuvi ya mwaka 1997 kwa ajili ya kulinda, kuendeleza, kukuza usimamizi endelevu wa rasilimali ya uvuvi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo. Jukumu hili ni zito na linahitaji ushiriki wa jamii mpana zaidi kama ililivyo ainishwa katika kifungu cha 25 (I) cha kanuni za uvuvi 2009.

Katika kutekeleza majukumu na usimamizi wa Sheria za Uvuvi kwa kipindi cha Julai 2016 hadi April 2017 Mkoa umeweza kukamata Zana Haramu na Wavuvi kama ifuatavyo:- Makokoro ya Sangara 1,113, Nyavu za Utali 9,346, nyavu za Dagaa 676, Kamba za Makokoro mita 169,896, Nyavu ndogo chini ya Inchi 6 4,454, Mitumbwi 87, Sangara wachanga 22,807 Kgs, Sato wachanga 342, Injini 2, Samaki wenye sumu 48.5, Nyavu za kuunganisha 332 Kgs huku Watuhumiwa 98 wakifikishwa Mahakamani na Watuhumiwa 71 walilipa faini na kupatikana jumla ya Shilingi 6,435,000.  Kutokana na usimamizi mzuri wa rasilimali za samaki kwa sasa kuna ongezeko kubwa la samaki kutokana na kupungua kwa vitendo vya uvuvi haramu.

Jedwali Na. 9: Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Doria mwezi Julai, 2016 hadi Aprili, 2017

WILAYA

MAKOKORO  YA SANGARA

NYAVU ZA UTALII

DAGAA NET

KAMBA  ZA KOKORO (M)

NYAVU NDOGO<6”

MITUMBWI

WATUHUMIWA

SANGARA WACHANGA (KG)

SATO WACHANGA

INJINI

FAINI

SAMAKI WA SUMU (Kgs)

NYAVU ZA KUUNGANISHA

WALIOLIPISHWA FAINI

WALIOFUNGULIWA MAHAKAMANINIANI

MUSOMA

144

741

29

37,533

1,698

61

53

52

8,361

0

2

6,435,000

30

82

RORYA

45

995

24

9,700

253

20

7

0

45

15

0

0

250

BUTIAMA

21

78

4

3,552

20

6

1

3

1,000

0

0

0

0

BUNDA

26

0

0

12,800

60

0

6

0

100

300

0

0

0

TARIME

0

0

0

0

0

0

0

0

400

0

0

18.5

0

JUMLA

236

1,787

57

63,585

2,031

87

67

55

9,906

315

2

48.5

332

HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA

 

178

904

273

-

-

-

-

-

-

-

-

-

-

-

NYAVU ZILIZOTEKETEZWA

 

149

2,564

24

78,674

150

-

-

-

-

-

-

-

-

-

NYAVU AMBAZO HAZIJATEKETEZWA

 

11

6

-

611

-

-

-

-

-

-

-

-

-

-

JUMLA

338

3,476

297

79,285

150

-

-

-

-

-

-

-

-

-

HALMASHAURI YA WILAYA YA RORYA

 

165

3,213

199

826

4

-

-

5

53

27

-

-

-

-

HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA DC

 

337

823

28

26,200

739

-

4

3

7,800

-

-

-

-

-

HALMASHAURI YA MJI WA BUNDA

 

37

47

95

-

1,530

-

-

35

5,048

-

-

-

-

-

JUMLA KUU

1,113

9,346

676

169,896

4,454

87

71

98

22,807

342

2

-

48.5

332




















Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 2017

    CHANGAMOTO

  1. Uchafuzi wa maji na makazi ya samaki kutokana na shughuli za kibinadamu pembezoni mwa ziwa ( kilimo na matumizi ya madawa ya kilimo karibu na ziwa, ukataji miti, uharibifu wa uoto wa asili kandokando ya ziwa unaofanywa na mifugo)
  2. Ukosefu wa vitendea kazi kama vile vifaa vya ukaguzi na upimaji wa ubora wa mazingira ya ufugaji wa samaki (maji na udongo), vifaa vya usafiri kwa ajili ya kuwatembelea wafugaji
  3. Ukame wa mara kwa mara unaozikumba Wilaya za Mkoa wa Mara hivyo kuathiri shughuli za ufugaji samaki.
  4. Maeneo mengi yenye sifa ya ufugaji kwenye vizimba (cage culture) kuwa maeneo tengefu na mazalia ya samaki.

       MIKAKATI

  1. Kuanzisha mabwawa/vitotoleshi na kuzalisha vifaranga bora wa samaki aina ya sato na kambale na kusambaza kwa wafugaji kwa gharama nafuu.
  2. Kuandaa/kuboresha utaratibu wa uvunaji na uuzaji wa samaki katika malambo ya vijiji yaliyopandwa samaki katika kipindi cha nyuma na yatakayopandwa samaki baadae ikiwa ni pamoja na utoaji wa vibali vya usafirishaji kwenye masoko.
  3. Kuhamasisha jamii katika vijiji vyote vyenye fursa ya ufugaji wa samaki kuanzisha na kuendeleza ufugaji wa samaki kwa kutoa mafunzo na elimu kwa vitendo kwa wafugaji na vikundi vya wafugaji katika maeneo husika.
  4. Kushirikiana na taasisi mbali mbali katika ulinzi wa rasilimali za uvuvi, kutoa elimu ya ugani na kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na viumbe wa majini.

Matangazo ya Kawaida

  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 MKOA WA MARA December 18, 2020
  • NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI, HISABATI, FUNDI SANIFU MAABARA NA LUGHA June 21, 2018
  • Mara yapaa Kimichezo July 20, 2019
  • JINSI YA KUPATA SALARY SLIP April 23, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mpango wa M-Mama watambulishwa Mara

    February 16, 2023
  • RC aitaka RUWASA kutoa taarifa ya vyanzo vya maji

    February 10, 2023
  • Nyanungu watakiwa kuitumia fursa vizuri

    February 10, 2023
  • RC avitaka vyama vya watu wenye ulemavu kuanzisha miradi

    February 10, 2023
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: P.o.Box 299 Musoma

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa