• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kilimo

Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 yalionesha kuwa Mkoa, ulikuwa na idadi ya wakazi 1,743,830 ambao wanaongezeka kwa asilimia 2.5 kwa mwaka. Hivyo, kwa maoteo ya idadi ya watu hadi Desemba 31, 2017 Mkoa unakadiriwa kuwa na watu wapatao 1,989,134. Kutokana na makadirio hayo, mahitaji ya chakula kwa mwaka 2017 yanakadiriwa kuwa tani 544,525 za mazao ya nafaka na mikunde.

 UTEKELEZAJI WA MALENGO YA KILIMO KWA MWAKA 2016/2017

Katika msimu wa kilimo 2016/2017, Mkoa ulikuwa na lengo la kulima jumla ya hekta 453,830 kwa lengo la kuvuna tani 1,008,649 za mazao ya chakula mchanganyiko. Kati ya hizo mazao ya wanga ni hekta 419,801 kwa lengo la kuvuna tani 972,879 na mikunde hekta 34,029 kwa lengo la kuvuna tani 35,770. Utekelezaji wa malengo ya kilimo cha mazao ya chakula mchanganyiko katika msimu wa vuli 2016/2017 unakadiriwa kufikia hekta 118,005 sawa na asilimia 42% ya lengo lililowekwa la Hekta 279,633 na makadirio ya mavuno kuwa tani 193,060 sawa na 24%, ikilinganishwa na lengo la tani 790,377 msimu wa vuli.

 

Jedwali Na. 8: Malengo ya kilimo na utekelezaji kwa mazao ya chakula katika msimu wa vuli 2016/2017

Aina ya Mazao

MALENGO

UTEKELEZAJI

%ya utekelezaji

HA

TANI

HA

TANI

HA

TANI

Mazao ya Wanga

259,109.7

760,149.55

109,344.29

190,037.39

42

25

Mazao ya Mikunde

20,523.3

30,227.45

8,660.83

3,022.75

42

10

JUMLA 

279,633

790,377

118,005.12

193,060.14

42

24

Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 2017

Katika Msimu wa masika 2016/2017, Mkoa umejiwekea lengo la kulima jumla ya Ha.335,824.88 kwa lengo la kuvuna tani 815,588.86  kwa mazao ya chakula mchanganyiko. Kulingana na hali ya hewa katika kipindi cha Masika kuwa ni ya kuridhisha kwa maeneo mengi Mkoa unatarajia kupata mavuno ya kutosheleza ambapo mazao mengi yapo katika hatua mbalimbali za kukomaa. Kwa ujumla, hali ya chakula bado kinapatikana ndani ya Mkoa hususan katika maduka, masoko / magulio ya vijiji, kata na maeneo ya baadhi ya Wilaya yameanza kuvuna mazao aina ya nafaka katika msimu wa vuli 2016/2017  kama vile Wilaya za Tarime na Serengeti

 UENDELEZAJI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Eneo la Mkoa linaloweza kumwagiliwa (Irrigation Development Potential) ni hekta 910,000, kati ya hizo uwezo wa juu (High potential) ni 210,100 Ha, uwezo wa kati (Medium potential) ni 576,500 Ha na uwezo wa chini (Low Potential) ni 123, 400 Ha. Jumla ya hekta 4,600 sawa na asilimia 2.2 ya eneo la uwezo wa juu (High potential 210,100 Ha) ndizo zinaendelezwa kwa kilimo cha Umwagiliaji. Kati ya hizo hekta 1,926 zimejengewa miundombinu bora na hekta 2,764 zinaendelezwa kwenye maeneo yasiyojengewa miundombinu bora ya umwagiliaji.

Baadhi ya maeneo yaliyoanza utekelezaji kwa kufanyiwa usanifu / kujengewa miundombinu ya Umwagiliaji ni bonde la Nyakunguru (katika Wilaya ya Tarime), Bonde la Mto Mara chini ya mradi wa NBI/NELSAP,  Ochuna, Rabuor, Chereche, Baraki “Sisters Farm’’, Chereche Singida, Irienyi (katika Wilaya ya Rorya), Mesaga, Bugerera, Kenyamonta, Nyamitita (Katika Wilaya ya Serengeti), Buswahili, Butiama (Wilaya ya Butiama), Masinono, Maneke, Chirorwe (Wilaya ya Musoma), Nansimo, Maliwanda, Nyatwali, Namuhula, Kisangwa na Bonde la Suguti  (Wilaya ya Bunda).  Miradi yote hii iko katika hatua mbali mbali za utekelezaji

 HUDUMA ZA UGANI

Kwa kipindi cha mwaka (2010/2011 - 2015/2016) pamekuwapo jitihada ya kuongeza wataalam wa kilimo ndani ya Mkoa, ingawa lengo halijafikiwa. Lengo ni kila kijiji kupata mtalaam wa ugani mwenye fani ya kilimo sambamba na Makao Makuu ya Mkoa / Wilaya watakaoweza kushughulikia masuala mtambuka katika kilimo kama vile Pembejeo, mazao ya biashara n.k. Hadi kufikia Desemba 2016, Mkoa ulikuwa na upungufu wa Wagani 197 katika ya mahitaji ya Wagani 628 kwa ajili ya kuhuduma maeneo hasa ya Vijiji na Kata.

PEMBEJEO NA ZANA ZA KILIMO

Katika msimu 2016/2017, Mkoa wa Mara umegawiwa Pembejeo zenye ruzuku ya tani 100 za mbolea ya kukuzia (Urea) na tani 50 ya mbegu za mahindi zenye jumla ya thamani ya Tshs. 319,500,000.00. Hata hivyo, Mkoa haukupata mbolea ya kupandia wala mbegu za Mpunga. Aidha, kulingana na mwongozo wa Pembejeo msimu 2016/2017 umeelekeza kamati za Pembejeo za Mikoa kutoa kipaumbele cha mgao kwenye maeneo yenye miundombinu ya umwagiliaji iliyokamilika.  Jumla ya wakulima 5,000 watanufaika na mbegu za mahindi ambapo wakulima 2,000 watanufaika na mbolea ya kukuzia. Matumizi ya Zana bora za kilimo yanaongezeka na hivyo, matumizi ya jembe la mkono yanapungua japo sio kwa kiasi kikubwa. Wakulima wanaotumia wanyama kazi kwa kulimia ni asilimia 37.08, wanaotumia Matrekta ni asilimia 4.75 na jembe la mkono hutumika kwa asilimia 58.17.

 CHANGAMOTO ZA JUMLA ZA SEKTA YA KILIMO

  1. Matumizi madogo ya zana bora za kilimo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji, usindikaji na tija.
  2. Kuendelea kujitokeza kwa visumbufu vya mazao hususani magonjwa ya mazao makuu ya chakula ya MLND, Batobato kali na Michirizi Kahawia hali inayosababisha baadhi ya maeneo kuwa uhaba wa chakula.
  3. Mabadiliko ya tabia Nchi ambayo yameathiri kwa kiwango kikubwa msambao wa unyeshaji mvua na kusababisha kalenda ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara Mkoani kutotambulika vizuri kwa wakulima wetu; na

MIKAKATI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO 

  1. Halmashauri za Wilaya kuhamasisha kwa bidii suala la ununuzi wa Zana bora za kilimo hususan matrekta sambamba na kuimarisha matumizi ya wanyama kazi.
  2. Halmashauri za Wilaya zinaendelea kutoa elimu kwa wakulima kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo, Chakula na Ushirika, Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru na Utafiti Mikocheni, kwa wakati kuhusu namna ya kudhibiti magonjwa ya “Maize Lethal Nicrosis Desease” MLND- (Mahindi) Batobato kali na Michirizi Kahawia kwenye zao la mihogo.
  3. Kila Wilaya kuwa na mipango bora na endelevu ya kununua, kuzalisha na kusambaza mbegu kinzani za muhogo kwa wakulima ili ifikapo msimu 2018/2019 kusiwe na mkulima anayepanda mbegu isiyo bora/kinzani.
  4.  Kuzitaka Halmashauri zitumie sheria ndogo katika kuwabana wakulima wasiotaka kufuata taratibu za kilimo bora ili waweze kudumisha kilimo chenye tija
  5. Kuendelea kuhamasisha Sekta binafsi ili kuwekeza katika usindikaji wa mazao ya kilimo kwa lengo la kupanua wigo wa soko la mazao.

Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • CCM yapongeza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Mara

    May 20, 2025
  • Kusaya awataka wahanga kutumia misaada kuboresha maisha

    May 19, 2025
  • BASATA yaijengea uwezo Mkoa wa Mara

    May 15, 2025
  • Mara kutumia fursa zilizopo kuboresha sanaa kwa vijana

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa