Jamal Zuberi
Musoma.
12 Julai, 2017
Serikali mkoani Mara imemtaka Makandarati wa ujenzi na Ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Ufundi kukamilisha kazi zote za msingi hadi ifikapo tarehe 25 Julai 2017 ili kuipusha usumbufu kwa wananfunzi kuendelea na masomo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara leo Dkt Charles Mlingwa baada ya kufanya ziara ya kujionea na kukagua ukarabati wa shule hiyo mjini Musoma
‘Ombi lenu la kutaka mkabidhi ukarabati huu wa shule tarehe 30 Julai 2017 nimelikataa hivyo nataka mkamilisha tarehe 25 Julai 2017 na nitarudi kuangalia hivyo, fanyeni kazi masaa 24 usiku na mchana hadi mkamilishe maeneo yote’ alisisitiza Dkt Mlingwa.
Amesema anataka kwa kipindi hicho kazi iliyobakia ya umalizaji ya kazi za ndani ya mabweni, madarasa, jiko na vyoo ikamilike haraka kwa lengo la kuwezesha wanafunzi tarehe 30 kufungua shule na kuanza masomo.
Awali akitoa taarifa ya mradi huo Mkuu wa Shule hiyo Mutta Jereniah alisema shule imepata jumla ya shs. Bili 1,2 kwa kupitia mpango wa Serikali kukarabati shule zote kongwe nchini. Alisema kuwa ukarabati huo unaosimamiwa na Chuo Kikuu cha Sayasi naTeknolojia cha Mbeya(MUST) ulianza rasmi mapema mwezi wa Juni 2017 mara baada ya shule kufungwa kwa ajili ya likizo
Ameyataji maeneo yanayofanyiwa ukarabati ni mabweni,madarsa,bwalo la chakula, jiko, ukumbiwa mikutano,jengola utawala, mabaara, vyoo, mabafu, mfumo wa maji safi na taka na umeme na mawasiliano.
‘ Jumla ya kazi iliyokwisha fanyika ni zaidi ya asilia mia 60 kwa mujibu wa msimamizi ambapo kazi kwa sasa ni za kumalizia kazi za ndani ya mabweni, madarasa jiko na vyoo ambazo haziwezi kuruhusu kafanyaika wakati wanafunzi wapo shuleni.
Shule ya Sekondari ya Ufundi Musoma ilianzishwa mwaka 1959 na ni ya michepuo wa sayansi na sanaa na ina jumla ya wanafunzi 986 kuanzia kidato cha 1 hadi VI.
MWISHO.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa